NECTA yaingilia kati madai ya mwanafunzi kubadilishiwa namba

0
340

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesema linafanyia kazi taarifa iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha mtahiniwa Iptisum Suleiman Slim wa shule ya Chalinze Modem Islamic Pre and Primary School akidai kubadilishiwa namba yake ya mtihani wakati anafanya mtihani wa kuhitimi elimu ya msingi uliofanyika tarehe 5 na 6 mwezi huu.