NECTA kinara katika usimamizi wa mitihani Afrika

0
257

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetajwa kuwa kinara Barani Afrika,
katika usimamizi wa mitihani na uendeshaji wa shughuli za kitaaluma na
hivyo kuwa mfano wa kuigwa.

Hayo yamesemwa na  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha alipotembelea ofisi za Baraza hilo zilizopo Mikocheni jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa NECTA, -Dkt Charles Msonde amewapongeza
Wafanyakazi wa Baraza hilo kwa mafanikio yaliyopatikana, ikiwa ni pamoja na kudhibiti uvujaji wa mitihani mbalimbali.