NEC yatangaza uchaguzi katika kata Sita

0
279

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa madiwani kwenye kata sita zilizopo kwenye mikoa sita ya Tanzania Bara.

Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage amesema kuwa uchaguzi huo utakaofanyika Mei 19 mwaka huu utahusisha kata za Uwanja wa Ndege mkoani Katavi, Kitobo mkoani Kagera, Kyela mkoani Mbeya, kata ya Mikocheni iliyopo mkoani Dar es Salaam, Mvuleni mkoani Lindi na Manda iliyopo mkoani Dodoma.

Amesema kuwa fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kati ya  tarehe  15 na 19 mwezi Aprili mwaka huu na uteuzi wa wagombea utafanyika  Aprili 19 mwaka huu, huku kampeni za uchaguzi zikipangwa kufanyika kuanzia tarehe 20 Aprili hadi tarehe 18  mwezi ei mwaka huu.

Kwa mujibu wa Jaji Kaijage, uchaguzi huo mdogo wa udiwani katika kata Sita za Tanzania Bara utafanyika pamoja na uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki.

NEC  imevikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo yanayotolewa na Tume wakati wa kipindi chote cha uchaguzi huu mdogo.