Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefanya mabadiliko ya uchaguzi mdogo wa Ubunge katika majimbo ya Muhambwe na Buhigwe mkoani Kigoma pamoja na kata 18 Tanzania Bara, ambao sasa utafanyika tarehe 16 mwezi Mei mwaka huu badala ya tarehe 2 mwezi Mei mwaka huu.
Akitangaza ratiba ya mabadiliko ya uchaguzi huo, Mkurugenzi wa uchaguzi wa NEC, – Dkt Wilson Mahera amesema kuwa kufuatia mabadiliko hayo, tarehe ya kuanza kuchukua fomu katika jimbo la Buhigwe ni 24 hadi 30 mwezi huu na kampeni zitaanza tarehe moja hadi 15 mwezi Mei.
Dkt. Mahera amesema kuwa, mabadiliko hayo yamefanyika ili uchaguzi katika majimbo ya Buhigwe, Muhambwe na kata 18 kumi ufanyike siku moja.
Jimbo la Buhigwe liko wazi kufuatia aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Dkt. Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na lile la Muhambwe liko wazi kufuatia kifo cha Mhandisi Atashasta Nditiye.