NEC yaanza maandalizi ya uchaguzi 2025

0
165

Serikali imesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ipo katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na hivyo itagawa majimbo ya uchaguzi kwa kuzingatia taratibu na vigezo vilivyoainishwa katika sheria wakati wa kugawa majimbo utakapofika.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge Ummy Nderiyananga ameliambia Bunge jijini Dodoma kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatoa tangazo rasmi kwa wadau wote wa uchaguzi juu ya kuanza kwa machakato wa ugawaji wa majimbo ili wadau wawasilishe maoni na maombi yao ambayo yatashughulikiwa kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa kikatiba.

Naibu Waziri Ummy alikua akijibu maswali ya Mbunge wa Kilindi Omar Kigua aliyetaka kujua ni lini Serikali italigawa jimbo la Kilindi lililopo wilyani Kilindi mkoani Tanga.