Ndugulile aitaka serikali kuondoa tozo Daraja la Kigamboni

0
122

Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile ameitaka serikali kuondoa malipo kwa vyombo vya moto vinavyovuka Daraja la Nyrere, maarufu Daraja la Kigamboni, na mzigo huo wa deni la NSSSF ubebwe na serikali.

Ndugulile ametoa rai hiyo bungeni jijini Dodoma akieleza kwamba nchini kote ni wakazi wa Kigamboni pekee wanaolipia kuvuka katika daraja lililojengwa na serikali yao.

Ameongeza kwamba wakazi wa Kigamboni hawana njia mbadala ya kutumia kama ambavyo wakazi wa Msasani, Masaki na wengine wanaotumia Daraja la Tanzanite, hivyo kuwatoza fedha ni kuwaumiza kudhorotesha juhudi zao za kujikwamua kiuchumi.

Daraja la Nyerere lilifunguliwa rasmi Aprili 19, 2016 na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ambalo lilijengwa kwa ushirika lati ya mfuko huo (60%) na serikali (40%).