Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amemtaka Mkandarasi anaesimamia ujenzi wa Hanga ya Ndege za Serikali katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kukamilisha ujenzi huo ndani ya siku 28.
Ndejembi ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam alivyofanya ziara ya kutembelea na kujionea ujenzi huo ambapo licha ya kuridhishwa nao lakini alimtaka mkandarasi ambaye ni Suma JKT kuongeza spidi kwani tayari yuko nje ya muda.
Tuna imani na mkandarasi kwa sababu ni Taasisi ya Serikali hivyo ilindeni Imani ambayo tumewapa, mliomba muongezewe siku 21 lakini mimi naongeza siku 28 ili mkamilishe hii kazi kwa weledi na ubora unaotakiwa,” Amesema Ndejembi.
Ujenzi wa Hanga hiyo ya Ndege za Serikali ambao matengenezo yote ya Ndege za Serikali, Maegesho ya Ndege za Serikali yatafanyika hapo ulianza katikati ya mwaka 2021 na kukamilika kwake kutagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.9.