Ndejembi atoa salamu za pole kwa familia ya Mzee Msuya

0
100

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Deogratius Ndejembi ni miongoni mwa waombolezaji wa msiba wa ndugu wa familia moja waliofariki dunia Agosti 02,2023 katika ajali ya gari Chalinze mkoani Pwani.

Katika Salamu zake Ndejembi amesema ameshiriki kwenye msiba huo kama jirani na sio kiongozi.

“Nipo hapa kama jirani, tumekuwa pamoja na familia hii ya mzee Msuya wengine hapa walituona tukivyokuwa, niseme tu Mama Msuya ndio alikuwa wa kwanza kuwa na duka mtaani kwetu, pipi na vitu vingine tulikuwa tunanunua hapo na hata familia yangu ilikuwa ikishirikiana na familia ya Mzee Msuya,” amesema Naibu Waziri Ndejembi.

Ndugu hao wa familia moja walioagwa leo mkoani Dar es Salaam ni Dkt. Norah Msuya, Sia Msuya na Diana Msuya na ni miongoni mwa ndugu wanne waliofariki dunia katika ajali hiyo.