Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limetekekeza agizo la Rais John Magufuli la kuanza safari kwenda mkoani Katavi.
Tayari ndege ya ATCL kutoka mkoani Dar es salaam kwenda Katavi imetua katika uwanja wa ndege wa Mpanda hii leo.
Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi amesema kuwa, kwa kuanza kutakua na safari moja kwa wiki ambayo itakua ni siku ya Jumatano kutoka Dar es salaam – kupitia Tabora hadi Mpanda na kurudi Dar es salaam na safari hiyo itakua ya muda wa takribani saa Mbili.
Oktoba Kumi mwaka huu akiendelea na ziara yake mkoani Katavi, Rais Magufuli aliiagiza ATCL kuanza safari zake mkoani Katavi kwa kuwa mkoa huo una fursa nyingi za kimaendeleo na aliongeza kuwa hataondoka mkoani humo mpaka ashuhudie ndege ya Shirika hilo ikitua mkoani humo.
