Mahakama Kuu ya Gauteng ya nchini Afrika Kusini, imetoa hukumu na kuamuru kuwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) iliyokua ikishikiliwa nchini humo iachiwe na mlalamikaji alipe gharama za kesi.
Ndege hiyo aina ya Airbus 220 – 300 imekua ikishikiliwa kwa muda wa wiki Mbili nchini humo na kusababisha Wanasheria pamoja na Viongozi kadhaa wa serikali kwenda nchini Afrika Kusini kushughulikia suala hilo.
Wanasheria na viongozi hao walikua wakiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharìki Dkt Damas Ndumbaro ambaye pia ni Wakili.