Ndege ya 8 kati ya 11 zilizonunuliwa na Serikali kuwasili leo

0
310

Rais John Magufuli, Leo anawaongoza Watanzania kupokea ndege
mpya ya Pili aina ya Boeing 787-8 Dreamline iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Ndege hiyo kubwa yenye uwezo wa kubeba abiria 262, inatarajiwa kutua majira ya mchana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikitokea nchini Marekani.

Hiyo inakuwa ndege ya Nane kati ya ndege 11 zilizonunuliwa na Serikali kwa lengo la kuiimarisha Kampuni ya Ndege Tanzania , kukuza Utalii pamoja na Uchumi.