Nchi zilizoendelea zatakiwa kuisaidia Afrika

0
226

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi ametoa rai kwa nchi zilizoendelea kuacha kutumia malighafi za Mataifa ya Afrika kuendeleza viwanda vyao na badala yake zisaidie nchi hizo kutumia rasilimali zake kujiletea maendeleo.

Profesa Kabudi ametoa rai hiyo huko  Yokohama, -Japan baada ya kushiriki mkutano wa Mawaziri wa maandalizi ya Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7).

Ameongeza kuwa wakati wa mkutano wao wamesisitiza umuhimu ya uwepo wa miundombinu ambayo inaunganisha nchi za Afrika ili kuziwezesha nchi hizo kuwa na miundombinu imara ya usafirishaji.

Profesa Kabudi ameongeza kuwa, mkutano huo pia umeazimia kuzitaka nchi zilizoendelea kuongeza fedha kwa ajili ya kutoa huduma za kijamii hasa katika sekta ya afya.

Akifungungua mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, -Kono Taro amezipongeza nchi za Afrika kwa kupiga hatua katika maendeleo kupitia ushirikiano na Japan.