Shirika la Afya Duniani (WHO) na washirika wake linatarajia kupeleka takribani dozi Milioni 18 za chanjo ya kwanza dhidi ya malaria iitwayo RTRTS,S/AS01 kwenye mataifa 12 ya Afrika.
Chanjo hiyo itakuwa imefikishwa kwenye mataifa hayo ndani ya kipindi cha miaka miwili ijayo.
Mataifa yatakayopata chanjo hiyo ni Kenya, Uganda, Burundi, Ghana, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Niger, Liberia, Benin, Cameroon, Burkina Faso na Sierra Leone.