NBC na mpango saidizi kwa wajasiriamali

0
140

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi amesema benki hiyo ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa akitaja njia wanazotumia kuwa ni kutoa elimu kwa wajasiriamali ya na mafunzo ya namna bora ya kutoa huduma bora kwa wateja pamoja na kuwapatia mitaji.

Akizungumza katika viwanja yanapofanyika maonesho ya 46 ya biashara kimataifa (Sabasaba) mkoani Dar es Salaam ameeleza kuwa wao kama taasisi ya kifedha wanashirikiana na wajasiriamali kwa kuhakikisha nao pia wanapata nafasi ya kutangaza biashara zao ili kupanua wigo wa biashara hizo.

Sambamba na hilo amesisitiza pamoja na kuwa na mitaji, biashara ya kisasa inahitaji ujuzi na matumizi ya teknolojia katika uzalishaji, hivyo benki hiyo inalitambua hilo na inaendelea kuwajengea uwezo wajasiriamali ili waweze kutumia fursa ya soko la Afrika na hata kuwa na nguvu ya kushindana katika soko hilo.