Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angellah Kairuki, ameuagiza Walaka wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kupitia upya nauli za mabasi hayo ili ziwe ni zile ambazo wananchi wa vipato vyote wanazimudu.
Waziri Kairuki ametoa agizo hilo mkoani Dar es Salaam alipokutana na kuzungumza na watumishi wa DART, wakati wa ziara yake ya kikazi katika taasisi hiyo.
Amesema DART inapaswa kuhakikisha kuwa inaweka viwango vya nauli ambavyo wananchi wa vipato vyote wanazimudu na si vinginevyo.
” Sisemi bei zifutwe, sisemi pia bei ziwe kiasi gani, lakini wataalamu warudi waangalie kwa jicho la kibiashara lakini wakati huo huo jicho la wananchi.” ameagiza Waziri Kairuki
Pia ameagiza kupitiwa kwa mikataba ya ubia ya uendeshaji wa mabasi kwa kuangalia vifungu vinavyohitaji utekelezaji ili utekelezaji ufanyike kwa wakati.