Nataka mzae : Rais John Magufuli

0
263

Rais John Magufuli amewashauri Watanzania kuendelea kuzaa na kuijaza nchi, kwa kuwa watu wengi ndio mtaji wa maendeleo ya Taifa.

https://www.youtube.com/watch?v=XlaBW32VifU&feature=youtu.be

Akihuhutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Majarida wilayani Tanganyika mkoani Katavi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo Rais Magufuli amesema kuwa nchi nyingi zilizoendelea kiuchumi Duniani ikiwa ni pamoja na China zina idadi kuwa ya watu.

“Maandiko yote yanasema nendeni mkazae, alafu anakuja mtu anawaambia msizae, ninajua Waziri wa Afya hili halifurahii lakini mimi nataka mzae, nikimaliza kipindi changu basi mfunge kuzaa, zaeni kweli kweli kwa sababu watoto tutawasomesha bure”, amesisitiza Rais Magufuli.