Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, – Juliana Shonza ameliambia Bunge kuwa matangazo ya Radio ya TBC Taifa yanapatikana katika wilaya 102 nchi nzima, huku msisitizo ukiwekwa kwenye wilaya zilizo pembezoni.
Akijibu swali na Mbunge wa Sikonge,- Joseph Kakunda kuhusu usikivu wa Redio ya TBC Taifa katika wilaya Sikonge na kwenye baadhi maeneo nchini, Naibu Waziri Shonza amesema kuwa, msisitizo uliowekwa na serikali kwa sasa ni kuongeza usikivu wa matangazo wa Redio ya Taifa kwa nchi nzima.
https://www.youtube.com/watch?v=WJjK5iVQTqw
Amasema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017, TBC imeongeza usikivu wa matangazo yake katika maeneo mengi ya pembezoni kwa lengo la kuwawezesha Wakazi wa maeneo hayo kupata taarifa mbalimbali kupitia Redio.
Naibu Waziri Shonza ameongeza kuwa, uwekezaji unaendelea kufanywa ili matangazo ya Redio ya TBC Taifa yaweze kuwafikia Wananchi wa Unguja na Pemba na maeneo mengine nchini.