Naibu Spika wa Bunge atangaza kugombea ubunge

0
568

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ameweka wazi kuwa atagombea ubunge, na kwamba wakati ukifika ataweka wazi atagombea jimbo lipi.

Dkt. Tulia ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma ikiwa ni siku moja kabla ya kuvunjwa kwa Bunge la 11 la Tanzania, ambapo wabunge na wananchi wengine watagombea kwa ajili ya kuwawakilisha mamiliona ya wananchi bungeni.

“Nami nimepata hamasa ya kujitosa. Na Inshallah Mwenyenzi Mungu atujalie uzima na afya, yumkini nitakwenda mahali fulani, kuomba ridhaa ya wananchi wenzangu,” amesema Tulia wakati akizungumza kuhusu mwenendo wa bunge

Aidha, kiongozi ameipongeza serikali kwa hatua mbalimbali ilizochukua kuhakikisha taifa linaendelea ikiwa ni pamoja na kuimarisha na kuboresha miundombinu, sekta za afya, utoaji wa elimu bure pamoja na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani.