Rais John Magufuli amemtembelea na kumjulia hali Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi ambaye amelazwa hospitalini.
Pamoja na kumjulia hali, Rais Magufuli pia ameshiriki dua ya kumuombea afya njema iliyoongozwa na familia ya Mzee Mwinyi.