Mzee Mkali azikwa

0
116

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuenzi na kuthamini mchango wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Mzee Hemedi Mkali kwa kujitoa kwake kwa maslahi ya Taifa tangu enzi za kupigania Uhuru.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Mzee Mkali yaliyofanyika Kiluvya, Dar es Salaam.

Akizungumza na mamia ya waombolezaji, Majaliwa amewataka Watanzania kuenzi yote mazuri aliyoyafanya Mzee Mkali enzi za uhai wake.

Mzee Hemedi Mkali alifariki dunia Julai 13, 2023 mkoani Dar es Salaam.