Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku amesema kuwa, kuna umuhimu kwa Watanzania kujitathmini ili kuona kama Wanaenzi na kuyaishi mambo ambayo yalikuwa yakisisitizwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
https://www.youtube.com/watch?v=wNIzQ8TtUaE&feature=youtu.be
Mzee Butiku ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati wa Tamasha la Sanaa la Mwalimu Nyerere, lililohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Wasanii.
