Mzee Bigambo arudisha tabasamu ya Waombolezaji

0
209

Mzee Samweli Bigambo, mkazi wa wilaya ya Chato mkoani Geita amesema ana imani Rais Samia Suluhu Hassan ataendeleza mambo yote ambayo yalianza kufanywa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt John magufuli.

Amesema Dkt Magufuli aliahidi kufanya mambo mengi, mengine yanawahusu Wakazi wa Chato ikiwa ni pamoja na kuifanya wilaya ya Chato kuwa mkoa, hivyo wangefurahi kama jambo hilo likatekelezwa.

Akizungumza katika Misa Takatifu ya Mazishi ya Dkt Magufuli huko Chato, Mzee Bigambo amesema Wanawake ni
Majasiri na wakiachiwa hakuna shaka mji wanauendeleza.

Amesema Chato wanashukuru Serikali kwa kumpa heshima kubwa Dkt Magufuli tangu siku alifariki dunia hadi siku ya kumlaza katika nyumba yake ya milele.

Pia ameiomba Serikali iendelee kuwa karibu na
Mjane wa Dkt Magufuli Mama Janeth Magufuli pamoja na familia yake, kwani anapitia katika kipindi kigumu.