Mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli umewasili katika visiwa vya Zanzibar ambapo hii leo mwili huo utaagwa na wakazi wa visiwa hivyo.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume mwili huo umepokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa na viongozi wengine wa serikali.
Mwili wa Dkt. Magufuli utapitishwa katika barabara za baadhi ya mitaa kuelekea Uwanja wa Amaan ambapo shughuli ya kuaga mwili huo itafanyanyika.
Mwili huo utapitishwa katika barabara Kiembe Samaki, Mombasa kwa Mchina, Mwanakwerekwe (round about), Amani kwa Mabata na kisha Uwanja wa Amaan.