Mwigulu: Wawekezaji ombeni mikopo

0
93

Wawekezaji wa ndani wametakiwa kuwasiliana na wizara ya Kilimo pamoja na wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kupata urahisi wa kupata mikopo kwa ajili ya kufanikisha uwekezaji.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na
Waziri wa Fedha na Uwekezaji Dkt. Mwigulu Nchemba kando ya mkutano wa Mifumo ya Chakula Barani Afrika kwenye majadiliano yaliyohusisha
wadau wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Amesema Serikali imeweka nguvu kubwa katika sekta hizo kwa kuwa zinazohudumia Wananchi wengi zaidi.

Waziri Nchemba ametoa wito kwa Wanawake na Vijana nchini kujiunga kwenye vikundi rasmi vya ujasiriamali Ili waweze kuwezeshwa kifedha Ili na hivyo kuwekeza kwenye Kilimo, Mifugo na Uvuvi.