Mwigulu aendelea kupatiwa matibabu

0
951

Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi lililopo mkoani Singida, – Mwigulu Nchemba anaendelea kupatiwa kwenye hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo mkoani Dodoma baada ya kupata ajali akiwa safarini katika barabara ya Iringa – Dodoma.

Madaktari wanaompatia matibabu Mbunge huyo wamesema kuwa hali yake inaendelea vizuri.

Taarifa za awali zinasema kuwa gari la Mwigulu limepata ajali ya kugonga Punda barabarani.