Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Geita Mhandisi Bahati Subeyaamesema barabara ya Sheli ya Nasoro – Hospitali ya Katoro – CCM iliyojengwa kwa
kiwango cha lami nyepesi iliyopo halmashauri ya Mji Mdogo wa Katoro itarahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii pamoja na kuchochea maendeleo ya wakazi wa eneo hilo.
Mhandisi Subeya amesema hayo wakati akitoa taarifa kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim, kuhusu lami nyepesi yenye urefu wa Kilomita 0.8.
Kabla ya kuzindua barabara hiyo, Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu alitoa rai kwa Wakazi wa eneo hilo kulinda miundombinu hiyo ya barabara.
Kaim amesema Serikal inatekeleza miradi mingi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo Wananchi, hivyo jukumu la Wananchi ni kuitunza miradi hiyo.
Barabara hiyo ya Sheli ya Nasoro – Hospitali ya Katoro – CCM iliyojengwa kwa
kiwango cha lami nyepesi imekamilika kwa asilimia Mia moja.
Ujenzi wake umegharimu shilingi Milioni 500 na imezinduliwa na Mwenge wa Uhuru unaoendelea na mbio zake mkoani Geita.