Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa mkoani Ruvuma baada ya kumaliza mbio zake mkoani Mtwara.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti amekabidhi mwenge huo kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika kijiji cha Sauti Moja wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Brigedia Jenerali Gaguti amesema ukiwa mkoani Mtwara, Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika wilaya tano na kuweka mawe ya
msingi, kuzindua, kuona na kukagua miradi 42 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 11.
Amesema miradi hiyo imetekelezwa na Serikali kwa kushirikisha nguvu za Wananchi.
Mkuu huyo wa mkoa wa Mtwara amesema miradi ambayo imebainika kuwa na kasoro atakaa na Watendaji wake, ili kufanya marekebisho na kuhakikisha miradi hiyo inatoa huduma bora kwa Wananchi.