Mwenge wa Uhuru unaenzi Falsafa za Baba wa Taifa: Waziri Mhagama

0
193

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, -Jenista Mhagama amesema kuwa Mwenge wa Uhuru utaendelea kukimbizwa nchi nzima ili kuenzi falsafa ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kujenga Umoja wa Taifa na kuchochea maendeleo.

https://www.youtube.com/watch?v=_qxr0BBr6og

Waziri Mhagama amesema kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa na faida kubwa katika kuchochea maendeleo ya Taifa, lakini pia umekuwa ni kichocheo cha Umoja na Mshikamano kwa Watanzania.

Waziri Mhagama ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali na Mbunge wa Viti maalumu, Mgeni Jadi Kadika aliyetaka kujua faida za kuendelea na mbio za Mwenge wa Uhuru badala ya kuuweka makumbusho ya Taifa.

Akijibu swali hilo Waziri Mhagama ameongeza kuwa, serikali itaendelea kuukimbiza kutokana na manufaa yake na pia ni kuenzi falsafa umoja na maendeleo ambayo iliasisiwa na Hayati Baba wa Taifa.

Mwenge wa Uhuru hukimbizwa nchi nzima kila mwaka na umekuwa ukizindua miradi mbalimbali ya maendeleo na pia umekuwa ukibeba kauli mbiu zenye kujenga Uzalendo na Umoja kwa Watanzania.