MWENDA ATEULIWA KAMISHNA MKUU ZRA

0
108

Yusuph Juma Mwenda ameteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) baada ya serikali kuridhia mabadiliko ya sheria ya kuanzishwa mamlaka hiyo kutoka ilivyokuwa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Saada Mkuya Saalum katika mkutano wake na wanahabari.

Amesema lengo la serikali kuridhia ZRB kuwa ZRA ni kujenga tasisi imara itakayoleta mtazamo chanya wa kiutendaji.