Mweka Hazina Kibondo asimamishwa kazi

0
736

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, – Thomas Chogolo, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma  zinazomkabili za ubadhilifu wa makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo.

Waziri Mkuu Majaliwa ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya  kikazi mkoani Kigoma.

 Amesema kuwa amefanya uamuzi huo kufuatia taarifa kuwa wananchi wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Kibondo  wamekua wakilipa kodi kupitia kwa watendaji wa kata katika maeneo yao, lakini  Mweka Hazina huyo amekua haingizi kwenye mfumo wa Serikali,  jambo ambalo halikubaliki.

Waziri Mkuu Majaliwa amesisitiza kuwa suala la ulipaji kodi ni nyeti na limepewa kipaumbele, hivyo ni lazima fedha inayokusanywa itumike kama ilivyokusudiwa ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miradi ya maendeleo.