Mwanasiasa mkongwe nchini Ibrahim Kaduma amefariki dunia nchini Indiausiku wa kuamkia hii leo, alikokuwa amekwenda kwa ajili ya uchunguzi waafya.
Mtoto wa marehemu, Imani Kaduma amesema kuwa, taratibu za kuurejesha nchinimwili wa baba yake kwa ajili ya mazishi zinafanyika nyumbani kwake Makongo Juu jijini Dar es salaam.
Enzi za uhai wake, Mzee Kaduma amehudumu katika nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje.