Mwambe aihama CHADEMA, ajiunga na CCM

0
381

Mbunge wa Ndanda kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Cecil Mwambe ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Mwambe ametangaza uamuzi huo katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam na kupokelewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.