Taharuki kubwa imewakumba wakazi wa mtaa wa Semtema A uliopo Manispaa ya Iringa baada ya kuibuka kwa Mwalimu mmoja anayewafundisha watoto masomo ya ziada (TUITION) kudaiwa kuwadhalilisha kijinsia wa watoto wa kiume wapatao (24).
Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa, Reinada Millanzi amesema mtuhumiwa huyo Anord Mlay maarufu kama BIG anashikiliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi wa kuwadhalilisha watoto hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 10 hadi 16 kwa nyakati tofauti nyumbani kwake.
Kamanda wa Milanzi amesema Mtuhimiwa huyo ni mhitimu wa Ualimu na anadaiwa kufundisha wanafunzi masomo ya ziada kwenye kibanda ambacho pia anakodisha miakanda ya Video (DVD)
Mkuu wa wilaya hiyo, Richard KaseselaI ametoa siku tatu kwa wananchi kutoa taarifa za watoto waliodhalilishwa ili watuhumiwa wachukuliwe hatua za kisheria.