Mvumbuzi wa Tanzanite afariki dunia

0
989

Mzee Jumanne Ngoma ambaye ni Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite yanayopatikana nchini Tanzania pekee katika eneo la Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara amefariki dunia leo jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na TBC, AfisaUhusiano Mwandamizi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminieli Eligaesha amesema Mzee Ngoma amefariki dunia wakati akiwa njiani kupelekwa hospitalini hapo.

Mwezi April mwaka 2018 Rais dkt. John magufuli alimpatia Mzee Jumanne Ngoma fedha kiasi cha shilingi milioni Mia Moja ili ziweze kumsaidia.

Mzee Ngoma alivumbua madini hayo mwaka 1967.