Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania -TMA imesema mvua zinatarajiwa kuendelea kunyesha katika mikoa ya ukanda wa Pwani hadi keshokutwa siku ya Jumapili.
Akitoa tathmini ya mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar Es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Samwel Mbuya amewataka wakazi wa mikoa ya ukanda wa Pwani kuchukua tahadhari.
Aidha amewatoa hofu wananchi kuhusu kimbunga Keneth.
Kamera ya TBC imepita katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar Es Salaam ikiwemo eneo la Kiluvya wilayani Ubungo baada ya kupata madai ya kukatika kwa miundombinu katika eneo hilo na kukuta hali ya usafiri ikiwa shwari na hakuna miundombinu iliyoharibiwa na mvua.
