Mvua kubwa, Radi na Upepo Kuikumba Mikoa 6

0
299

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza mvua kubwa katika Mikoa sita ya Tanzania Bara na baadhi ya maeneo Visiwa vya Unguja na Pemba zitakazodumu kwa siku tano kuanzia leo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Wilberforce Kikwasi amesema mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa Jijini Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Mikoa ya Kusini pamoja na Unguja na Pemba ni za siku tano mfululizo.

Kikwasi amewataka wananchi wa maeneo yanayozunguka Mikoa hiyo kuchukua tahadhari

“Hali hii ya mvua inatokana na kuendelea kuimarika kwa ukanda wa mvua katika maeneo ya Kusini mwa nchi na hivyo kusababisha kujengeka kwa mawingu makubwa na mazito yanayosababisha mvua kubwa zitakazoambatana na upepo mkubwa na radi” amesisitiza Kikwasi