Mvua kubwa kunyesha kuanzia  kesho  

0
275

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imetangaza kuwepo kwa mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika ukanda wa Pwani kuanzia tarehe tatu hadi tano mwezi huu.

Taarifa ya TMA iliyotolewa mkoani Dar es Salaam imeeleza kuwa licha ya mvua hizo kubwa kumalizika tarehe tano mwezi huu, mvua za kawaida zitaendelea hadi mwezi Aprili mwaka 2022.
 
Kufuatia uwepo wa mvua hizo, TMA imewataka Watanzania wote kuchukua tahadhari hasa kwa mvua zinazoambatana na radi.