Kivuko cha MV Magogoni kinachotarajiwa kuanza kukarabatiwa mara baada ya kusainiwa kwa mkataba wa ukarabati hii leo katika viwanja vya Kivukoni jijini Dar es Salaam.
Kivuko hiki kina uwezo wa kubeba abiria elfu mbili na tani 500 za mizigo yakiwemo magari madogo 60 kwa wakati mmoja.
Kivuko cha MV Magogoni kina urefu wa mita 72.5, upana wa mita 17.4 na kina cha kuelea (draft) mita 1.7.