Musukuma aamsha shangwe Bungeni

0
119

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Musukuma ameamsha shangwe ndani ya ukumbi wa bunge jijini Dodoma, baada ya kusimama na kuuliza swali kwa lugha ya Kiingereza kwa mgombea Ubunge wa Afrika Mashariki Mhandisi Mohamed Mnyaa.

Baada ya Spika Tulia Ackson kumtaja Musukuma kuuliza swali kwa mgombea huyo, wabunge wameibua shangwe na kugonga meza huku baadhi wakimtuza fedha kutokana na umahiri wake wa kuulizwa swali kwa lugha ya kiingereza.

Mbunge Musukuma amemuuliza Mnyaa kuwa “kwa kipindi cha miaka mitano amefanya nini mpaka aombe tena kuchaguliwa katika Bunge hilo?.”

Hata alivyotakiwa kurudia tena swali hilo bado Mbunge huyo alikua na ujasiri na kuuliza.

Mara kadhaa Mbunge Musukuma amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisema elimu yake ni darasa la saba, lakini ana uwezo mkubwa kulinganisha na wale wanaojiita wasomi.