MUST kupatiwa Shilingi Bilioni 2.5

0
584

Rais John Magufuli ameahidi kukipatia Shilingi Bilioni 2.5 Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya –  MUST mwezi huu wa Mei  ili kiweze kukamilisha mradi wa ujenzi wa Maktaba ya chuo hicho.

Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo baada ya kuweka jiwe msingi la ujenzi wa Maktaba ya chuo hicho,  ambapo Makamu Mkuu wa MUST,  -Aloys Mvuma alimueleza kuwa ujenzi wa Maktaba hiyo umekua hauendi kama ilivyotarajiwa kwa kuwa bado Mkandarasi hajalipwa kiasi cha pesa kilichobaki.

Hata hivyo Rais Magufuli ameshangazwa na hatua ya chuo hicho ya kutafuta Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa Maktaba hiyo, wakati wana Wataalamu wa kutosha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo kwa ufanisi.

Ujenzi wa Maktaba hiyo mpya  ya  Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya,  utagharimu Shilingi Bilioni 5.5 na mpaka sasa tayari Shilingi Bilioni 2.9 zimekwishatolewa.

Awali Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prosea Joyce Ndalichako alimueleza Rais Magufuli kuwa Maktaba iliyopo  sasa ina uwezo wa kutumiwa na Wanafunzi 150 na Maktaba mpya inayojengwa itakua na uwezo wa kutumiwa na Wanafunzi Elfu Mbili na Mia Tano.