Muroto ataka wahalifu wa mitandao kudhibitiwa

0
258

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma, – Gilles Muroto ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Kanda ya Kati kushirikiana na kampuni za simu kuwadhibiti wahalifu wanaotumia mitandao kuwaibia wananchi.


Kamanda Muroto ametoa wito huo jijini Dodoma, wakati akifungua mkutano wa wadau wa huduma za mawasiliano kutoka mkoani humo, mkutano unaojadili namna ya kuwadhibiti wahalifu wanaotumia mitandao.


Amesema kuwa endapo hali hiyo isipodhibitiwa kwa sasa, italeta madhara makubwa katika siku zijazo, kwa kuwa watu wanaofanya vitendo hivyo wamekua wakitumia mbinu mbalimbali.


Baadhi ya wadau hao wa huduma za mawasiliano mkoani Dodoma ambao wanashiriki mkutano huo wameahidi kushirikiana na TCRA pamoja na Jeshi la Polisi ili kuwabaini wahalifu hao wanaotumia mitandao.