Mufti: Dkt Magufuli alikuwa mzalendo na mwenye utu

0
323

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amesema Rais wa awamu wa tano Hayati Dkt. John Magufuli alikuwa ni kiongozi anayejali utu, usawa na hakuwa mbaguzi.

Amesema wakati wa uhai wake Dkt. Magufuli alikuwa akiwajali sana wengine na alipenda zaidi kuwasaidia wanyonge kupata haki zao, jambo ambalo linasisitizwa na dini zote

Kwa upande wa Viongozi wa dini, Mufti amesema kuwa Hayati Dkt. aliwapenda na kuwajali sana, hali iliyowafanya waone kuna umuhimu wa wao kushirikiane naye katika masuala mbalimbali ya Kitaifa.

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir ameyasema hayo mkoani Dodoma, wakati wa kongamano maalum lililoandaliwa na Viongozi wa dini ili kumshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Dkt. Magufuli.

Amesema Hayati Dkt. Magufuli alikuwa Mzalendo wa kweli kwa Taifa lake, na hivyo hali kuwafanya anaowaongoza wafuate nyayo zake.