Mufti Aipongeza JUVIKIBA

Mufti Day

0
151

Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania Aboubakar Zubeir bin Ali ameipongeza Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu BAKWATA Taifa (JUVIKIBA) kwa kuandaa mashindano ya kuhifadhi Quran kwa vijana wadogo pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali ikiwemo kompyuta mpakato (laptop) baiskeli, vyerehani, mabegi pamoja na fedha taslim

Akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa na JUVIKIBA Mufti amesema ataendelea kuwaamini vijana na kuwapa fursa za kujiendeleza kielimu , kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili kusaidia Jumuiya hiyo na kukuza kizazi kilicho bora kwa manufaa ya Taifa zima

Hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya BAKWATA vilivyopo Kinondoni mkoani Dar es salaam imehudhuriwa na Mgeni Rasmi Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Mohamed Gharib Bilal