Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir atoa wito kwa Waumini wa dini ya Kiislamu na wale wa dini nyingine kuchangia shughuli za maendeleo.
Mufti ametoa kauli hiyo mkoani Mwanza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti wa Shamsiyat Bakwata Kilumba, uliopo wilayani Ilemela.
Amewataka watu wote wenye nia njema bila ya kujali dini zao, kuchangia ujenzi wa msikiti huo.
Ujenzi huo utakapokamilika , jengo hilo la msikiti wa Shamsiyat Bakwata Kilumba, litakua na ghorofa Mbili.
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir, pamoja na Waumini wengine wa dini ya Kiislamu, wapo mkoani Mwanza kwa ajili ya Sherehe za Maulid.