Mtumishi wa TBC apewa zawadi

0
197

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba Chacha amemkabidhi pikipiki mfanyakazi wa shirika hilo Sunday Nkayamba,
ikiwa ni zawadi kwa uzalendo wake na kujitoa kwa maslahi ya shirika.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za TBC Mikocheni mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hiyo Dkt. Rioba amewataka wafanyakazi wengine wa TBC kuiga mfano wa Sunday kwa kuwa wazalendo na Shirika lao na Taifa kwa ujumla.

Akipokea pikipiki hiyo Sunday amemshukuru Dkt. Rioba kwa kuthamini mchango wake katika shirika hilo la Utangazaji Tanzania.