Mtanzania ashinda Tuzo ya Nobel

0
236

Profesa Abdulrazak Gurnah ambaye ni Mtanzania, ameshinda Tuzo ya Nobel katika Fasihi kwa mwaka 2021.

Profesa Gurnah alizaliwa visiwani Zanzibar mwaka 1948 na kuhamia nchini Uingereza akiwa mdogo.

Hadi sasa amechapisha riwaya 10 ambazo nyingi zimeangazia athari za ukoloni na changamoto za Wakimbizi.

Profesa Gurnah amekuwa akifundisha lugha ya kiingereza pamoja na fasihi katika chuo kikuu cha Kent na Canterbury kabla ya kustaafu hivi karibuni.

Anakuwa mwandishi wa pili kutoka Barani Afrika kushinda tuzo hiyo ambapo mwaka 1986 Wole Soyinka kutoka nchini Nigeria alishinda.