Mtandao wa wizi wa magari wanaswa Njombe

0
185

Jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia watu watano wanaodaiwa kuhusika na mtandao wa wizi wa magari nchini ambao wamekutwa na magari Saba yanayosadikiwa kuibwa katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya na Singida.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Njombe, – Hamis Issah amesema wezi hao wamekuwa wakiiba magari na kuyabadilisha rangi na kubadili namba za injini.

Kamanda Issah amewataja Watuhumiwa hao wa wizi wa magari kuwa ni Edrick Hussein maarufu kwa jina la Kimya Kimya mkazi wa jijini Dar es salaam, Sudi Abuba Mwinyi mkazi wa Uyole Mbeya, Method Mkongwa mkazi wa Njombe, Imani Fidelis mkazi wa Moshi Kilimanjaro na Timoth Nehemia mkazi wa Mufindi.
 
Watuhumiwa hao pia wamekutwa na vifaa mbalimbali vya magari na ufundi wa magari vinavyodhaniwa kutumika katika wizi.