Mkuu wa wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, – Asumpta Mshama ameagiza kukamatwa msimamizi wa kiwanda cha kutengeneza nyuzi za hariri cha Sunda Chemical Fiber, raia kutoka nchini China kwa tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwapiga na kuwaumiza Wafanyakazi wake wakiwa kazini.
Mshama ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara ya kukagua kiwanda hicho baada ya kutokea matukio mawili ya kutisha ya mfanyakazi mmoja kuunguzwa mguu kwenye tanuru la maji ya moto na mwingine kusukumwa na kuanguka chini kutoka ghorofa ya Tatu.