MSD yaagiza mashine ya kusafisha damu

0
193

Bohari ya dawa nchini MSD imeagiza mashine za kusafisha damu kutoka kwa watengenezaji ili kuwezesha upatikaji wa huduma hiyo Kwa gharama nafuu na rahisi kwa wagonjwa wa figo hapa nchini.

Mratibu wa Magonjwa ya Figo, kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Linda Ezekiel amewaambia waandishi wa habari kwenye mafunzo jijini Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya siku ya figo, Machi 10 mwaka huu.

Dkt. Ezekiel amesema wagonjwa wa figo wamekuwa wakikabiliwa na gharama kubwa ya huduma hizo serikali kupitia Bohari Kuu dawa MSD tayari imeagiza mashine 171 za kusafisha damu na mashine za kuchakata maji 11.

Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa awamu ya sita, serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilion moja katika huduma za usafishaji damu zipatikane katika hospitali zote nchini.

Dkt. Linda amesema takwimu zinaonyesha takribani wagonjwa 1000 wana matatizo ya figo nchini.

Amesema kati ya wagonjwa  5800 na 8400 wanaohitaji huduma ya kusafisha damu, 2750 tu wanapata huduma hiyo.

Kwa sasa hospitali ya Taifa ya muhimbili inahudumia wagonjwa 200 hadi 300 Bugando 150 Agakhani 25 na hospitali ya Regency wagonjwa 40.

Naye Mdhibiti Ubora kutoka Bohari kuu ya Dawa(MSD) Josepgh Kitukulu amesema kuwa serikali inatumia zaidi ya billion 29,484  kwa mwaka kufanya huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa 1000.

Katukulu amesema  kupitia Bohari Kuu ya Dawa itaokoa   zaidi ya bilioni 13 na hivyo kuboresha upatikanaji wa huduma zinazoambatana na hizo.

Kila ifikapo tarehe 3 mpaka 7 kila mwaka, Tanzania inaungana na nchi nyingine kuadhimisha siku ya figo duniani.