Mratibu wa Tarura Rukwa asimamishwa kazi

0
244

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amemsimamisha kazi Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura) mkoa wa Rukwa, Mhandisi Boniface William, ili kupisha uchunguzi kufuatia malalamiko kuwa amekua akifanya upendeleo wa katika kutoa kandarasi za ujenzi wa barabara za mkoa huo.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo Mjini Sumbawanga, wakati akizungumza na Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilolitoa hapo jana akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Aidha waziri Jafo ametumia mkutano huo kuziagiza halmashauri zote nchini, kuhamia kwenye maeneo yao ya Kiutawala ili kuwa karibu na Wananchi.